Tuesday, 26 August 2014

Punguza mafuta a.k.a unene mwili kwa njia rahisi

Punguza mafuta mwilini (Lose weight fast Program) 
Njia moja ya haraka ya kupunguza uzito haraka ndani ya muda mfupi. Unaweza ukapunguza kilo 7 hadi 10 ndani ya mwezi kama ukifanya zoezi hili.
Acha kula vyakula vya mafuta, wanga uliokobolewa pamoja na matumizi ya sukari kupita kiasi.
Nini unapaswa kula
  1. Kiazi kitamu
  2. Green Tea
  3. Apple
  4. Maji ya uvuguvugu
  5. Mboga za majani
Namna ya kuandaa au kula vyakula hivi:
Asubuhi:
  • Kunywa maji ya moto utakapoamka
  • Kula apple dk 15 kabla ya kupata chai
  • Kunywa chai itokanayo na green tea
  • Vitafunwa viwe viazi vitamu
  • Usinywe maji mara baada ya kunywa chai. Pata maji ya uvuguvu dk 30 baada ya kupata chai
Mchana
  • Pata maji ya uvuguvugu dk 30 kabla ya kupata mlo wa mchana
  • Pata apple dk 15 baada ya kunywa maji ya uvuguvugu
  • Kunywa chai (green tea) na kiazi kitamu.
  • Unaweza kula pamoja na mboga za majani kwa wingi
  • Maji ya uvuguvugu yanywe baada ya dk 30 tangu ule chakula cha mchana
Jioni:
Mlo wa jioni upate kama ulivyopata mlo wa mchana. ikiwezekana pata mlo wa jioni kabla ya saa 2. Yaani ifikapo saa 2 jioni uwe umeshapata mlo wa jioni.
Kuondoa mafuta na sumu kila siku
Mahitaji:
  1. Asali mbichi: kijiko 1 cha chai
  2. Mdalasini: ½ kijiko cha chai (unga wa mdalasini)
  3. Limau: Vijiko 2 vya chai (juice ya limau isiyochanganywa kitu)
  4. Maji: Glasi 1 (yasiwe ya moto yasiwe ya vuguvugu – yawe ya kati)
Zoezi hili lifanyike asubuhi na mapema kabla hujala chochote (tumbo likiwa tupu).

Maandalizi:
  1. Weka unga wa mdalasini ndani ya chupa ya chai
  2. Chemsha maji (hakikisha yanakuwa glasi moja baada ya kuchemshwa), kisha mimina kwenye chupa y chai yenye unga wa mdalasini.
  3. Acha mchanganyiko huu ukae kwa muda wa nusu saa ili mdalasini ukolee kwenye maji.
  4. Mimina mchanganyiko huo kwenye glasi au kikombe.
  5. Ukishapungua joto, changanya weka asali mbichi, pamoja na juice ya limau.
  6. Sasa waweza kunywa mchanganyiko huo.
  7. Pata mlo saa moja baada ya kunywa mchanganyiko huo
Waweza rudia kunywa mchanganyiko huu, usiku unapokwenda kulala



No comments:

Post a Comment