AMA
kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful
Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha)
kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’,
umekosea sana kwani upepo umegeuka.
Habari
za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala
anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wote kwa maana ya
kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na
Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi
cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo
kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga
kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala
ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa
analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya
Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo
vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya
ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na
anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh.
milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
Akizungumza
na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo
amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa
akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa
na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya
biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo
yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Utafiti
umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa likiwemo la
kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu ambalo ni Toyota Harrier.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
Akizungumza
na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina , rafiki wa karibu wa
Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi
tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali
na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam
kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa
zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule
alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
Hivi
karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema,
walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
Baada
ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo
yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa
na kiuchumi.
“Kama
kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza
akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume,
jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini
jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaoni.
No comments:
Post a Comment