MBUNGE
wa Vunjo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Augustine
Mrema (TLP), amesema kuna haja Rais Jakaya Kikwete aongezewe muda wa
kuongoza nchi.
Alisema kama Rais Kikwete ataongezewa muda, atapata muda wa kukamilisha mchakato wa Katiba ambao ndiye aliyeuanzisha.
Mmoja
wa wajumbe waliohudhuria kikao kati ya Rais Kikwete na Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD) kilichofanyika mwanzoni mwa wiki Ikulu ndogo
ya Kilimani mjini Dodoma, aliiambia MTANZANIA kwamba Mrema aliyasema hayo alipokuwa akichangia wakati wa kikao hicho.
“Wakati
mjadala unaendelea, Mrema alipendekeza Rais Kikwete aongezewe muda wa
mwaka mmoja au miwili ili afanikiwe kukamilisha mchakato huu wa Katiba.
“Alipotoa
pendekezo hilo, kuna mjumbe mmoja akamuuliza, ‘sasa Mrema unataka muda
uongezwe ili na wewe upate muda wa kupambana na Mbatia (James Mbatia,
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) anayekusumbua kule Vunjo au?’
“Huyo mjumbe alipouliza hivyo, Mrema akadakia na kusema, ‘hapo hapo’,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa .
Chanzo
hicho kilisema kuwa Mrema aliendelea kumsihi Rais Kikwete amzuie Mbatia
asiende Vunjo kwa kuwa anapokuwa huko anatumia jina lake, kwamba
amemtuma kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Mbatia
alipozungumza na MTANZANIA kwa simu jana juu ya malalamiko hayo,
alisema hawezi kuendelea kujibizana na Mrema kwa kuwa ni mkubwa wake.
“Mimi
sikulelewa katika mazingira ya kujibizana na wakubwa zangu ila
ninachosema ni kwamba, wakati wa mkutano wangu wa hadhara niliohutubia
Vunjo wiki iliyopita, wenyeviti 11 wa serikali za vijiji walioshinda
kupitia TLP, wenyeviti 32 wa vitongoni ambao ni wa TLP, msaidizi wa
Mrema pamoja na wanachama wapya 1,564, walihamia NCCR-Mageuzi,” alisema Mbatia.
No comments:
Post a Comment