Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza nchini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito.
Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba wake aitwae Charlotte kuwa mjamzito, mtandao wa Itv news umeeleza.
Habari
zinasema mwanaume huyo mwenye miaka 29 anayefanya kazi ya ulinzi
,amesema ameongezeka uzito na tumbo limekua mithili ya aliye mjamzito na
kudai kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na cha ajabu amekuwa na
hamu ya baadhi ya vyakula.
Harry ameripotiwa kuwa na dalili za kuwa mja mzito miezi miwili baada ya kubaini kuwa mchumba wake ni mjamzito.
Harry amekuwa akipatiwa dawa na inasemekana anaweza kudai mafao wakati akiwa katika mapumziko hayo.
No comments:
Post a Comment