Wizara ya maliasili na utalii
imewasimamisha kazi watumishi wake ishirini na mbili wa idara ya wanyama
pori wanaotuhumiwa kushiriki katika vitendo vya ujangili dhidi ya
wanyama pori, hujuma, pamoja na vitendo vya rushwa na hatua za kisheria
zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh. Lazaro
Nyalandu amesema watumishi waliosimamishwa 11 wanatoka kikosi dhidi ya
ujangili Arusha, 4 pori la Akiba Rukwa-lwafi,1 kikosi dhidi ya ujangili
Bunda,3 pori la Akida Maswa,1 pori la akida Selous na 1 mapori ya akida
Lukwika -Lumesule Msanjesi na kuongeza kuwa wote hao uchunguzi wa kina
ulifanyika na kuwabaini kuhusika na vitendo hivyo huku akisisitiza hatua
kali zitachukuliwa kwa mtumishi yeyote atakayetumia wadhfa wake
kuhujumu rasilimali za taifa.
Aidha ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa
kushirikiana na wizara imemkamata askari wa wanyamapori mkoani Singida
aliyejehusisha na vitendo vya ujangili akiwa na bunduki mbili na ndege
12 aina ya Flamingos nyumbani kwake kinyume cha sheria na tayari
ameshasimamishwa kazi na hatua za kumfikisha mahakamani zinachukuliwa
ili ajibu tuhuma hizo.
Nao baadhi ya wananchi licha ya kupongeza hatua
hiyo wamesema serikali inapaswa kutambua mtandao unaotumika ni mkubwa
hivyo kuongeza jitihada zaidi kwa kutenda haki ili wale wote
watakaobainiki kuhusika wawajibishwe.
No comments:
Post a Comment