Mwenyekiti
wa Kamati ya Vijana Wapenda Amani Tanzania, Said Mwaipopo (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara
ya habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam Januariy 8-2014,kupinga
mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpya kuwepo kwa serikali tatu. Kushoto
ni Katibu wa kamati hiyo, Chifu Msopa.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
…………………………………………………………………..
Kuanzia
tarehe 11.01.2014 Matembezi ya hiyari kwa miguu kutoka Dar es Salaam
mpaka Morogoro yataanza rasmi yakikadiriwa kuchukua siku zisizozidi
kumi, lengo kuu likiwa ni kuhamasisha, kukumbushana na kuenzi Umoja,
Amani na Utulivu kama Taifa moja likaitwa Tanzania
ilhali juhudi yakinifu kuanzia ngazi ya mwananchi mmoja mmoja, familia,
kaya, wilaya mpaka Taifa kujivika jukumu la kufahamu, kupambanua,
kudadavua na mwisho wa siku kushirikiana kupitia njia za makusudi
kuhakikisha maliasili na utajiri wa Taifa hili jadidu unamnufaisha kila
Mtanzania, huku masuala ya Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Ujasiriamali na
Taaluma yakitiliwa mkazo pasi kuachwa kando.
Matembezi
haya yanatarajiwa kuwa na vituo kadhaa vikiwemo ; Kibaha, Mlandizi,
Vigwaza, Chalinze, Mikese na kumalizia Morogoro, tunatarajia ndugu zetu
Watanzania tujikimu kwa mahitaji kadha wa kadha tuwapo safarini, Nchi
ikiwa Yetu, Wajibu ukiwa Wetu na UTAIFA tukiuweka na kuutanguliza mbele.
Mpaka
sasa matembezi haya ya hiyari yenye kauli mbiu Nchi Yangu, Wajibu Wangu
: UTAIFA KWANZA hayajapata mdhamini yeyote na maandalizi yote mpaka
sasa ni kufikia lengo la matembezi kama Tanzania iliyo moja bila kujali
itikadi, imani, dini, asili ama hata tofauti za kiuchumi miongoni mwetu
na kuangaza katika Tanzania yenye kutoa nafasi kwa kila Mtanzania.
Kwa
hakika maandalizi ya msingi yamekamilika na tarehe 11.01.2014 ndoto
yetu ya kufanya matembezi ya hiyari yatafikisha ujumbe ulio wa Amani na
Ustawi wa Taifa letu itachukua nafasi na kuwa halisia.
Nchi Yangu, Wajibu Wangu : UTAIFA KWANZA
No comments:
Post a Comment