Said Fella 'Niseme Nisiseme'
Kikundi
maarufu cha wasanii wa muziki nchini 'Mkubwa na Wanawe' aka Yamoto Band
kipo mbioni kuzindua kichupa chao kipya kilichobatizwa jina 'Niseme
Nisiseme'.
meneja wa TMK Wanaume Family Said Fella akiwa na Mkubwa na wanawe 'Yamoto band'
Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family na kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella ameongea na eNewz kuwa hii ni moja ya video
mpya inayotarajiwa kutambulishwa wiki hii ndani ya Tinga' Namba Moja
kwa Vijana (EATV) iliyofanywa na watayarishaji mahiri Pablo na Iri.
Fella
ameongezea kuwa uzinduzi wa wimbo huo utafanyika Jumapili Jijini Dar es
Salaam ambapo pia wamepanga kutoa "Surprize" nyingi kwa mashabiki wao
na pia listi nzima ya wasanii watakao perform siku hiyo itatangazwa wiki
hii.
No comments:
Post a Comment