Tuesday, 26 August 2014

WAHADHIRI UDSM WAPANDISHWA NGAZI

 
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),  umewapandisha hadhi baadhi ya wahadhiri kuanzia Julai mosi mwaka huu.
Afisa Uhusiano wa chuo hicho,  Jackson Isdory,  alitaja baadhi ya vyeo ambavyo wahadhiri hao wamepewa kuwa ni uhadhiri uandamizi, usaidizi na uprofesa kwa kuangalia vigezo vya kazi zilizofanywa kwa mwaka husika aliyepandishwa hadhi  zikiwamo  utoaji wa machapisho mengi yaliyoandaliwa kiustadi na tafiti nyingi.

Waliopandishwa hadhi kuwa maprofesa ni Shadrack Mwakalila kutoka Idara ya Jiografia katika Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii (CASS) na Agnes Mwakaje kutoka Taasisi ya Tathmini ya Rasilimali ambaye ametoa machapisho 16.

Waliopandishwa hadhi kutoka uhadhiri mwandamizi kuwa Maprofesa waandamizi ni Godius Kahyarara,  Wily Komba, Kitila Mkumbo, Sylevester Lyantagae,  Eliot Niboye, Eshther Dungumaro na Aldin Mutembei wa Taasisi ya Masomo ya Kiswahili.

Wengine ni Abraham Temu, Shukrani Manya, Wineaster Anderson kutoka Idara ya Masoko na Chuo cha Biashara-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alisema kamati yenye mamlaka ya kuteua imewapandisha hadhi wahadhiri saba kutoka uhadhiri kwenda uhadhiri  uandamizi wakiwamo  Christine Noe, Alexander Makulilo, Tumsifu Ely, Severine Kessy, Bruno Nyundo, Stephen Maluka na  Pendo Malangwa.

Pia wahadhiri wasaidizi watatu wamepandishwa kuwa wahadhiri kamili ambao ni Robert Suphian-Idara ya Masoko, Hashim Uddi wa Idara ya Umeme na Uhandisi wa Mwasiliano, Angelius Mnenuka na Advetina Buberwa  wote kutoka Taasisi ya Masomo ya Kiswahili.
 

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment