Wanasaikolojia wakiongozwa na mwanasaikolojia Benedict Jones wamegundua kwamba, mwanamke akitaka kupima uzuri wa mwanaume ambaye angependa kuwa rafiki au mpenzi wake, hupenda kujua kama hata wanawake wenzie wanampenda kama yeye anavyompenda……..
Anavyozidi kuwaona wanawake wenzie
wakitabasamu au kumchekea mwanaume huyo anapopita mbele yao ndivyo
atakavyojua kwamba, huyo mwanaume ni mzuri.
Hali hii inafahamika kama copycat reflex
na ni matokeo ya nadharia ya Darwin ya mambo ya mabadiliko ya maumbile
ya viumbe, kwa mujibu wa wataalamu hao, yaweza kutumika pale ambapo
mwanamke anakumbana na wanaume wengi wanaomtaka lakini anapata matatizo
ya kumchagua yupi na kumwacha yupi.
Au akiona uchaguzi wa mwanaume bora
utamchukulia muda wake mwingi na nguvu zake hujirahisishia kwa kuchukua
uamuzi wa kuwaangalia wanawake wenzie wanavyomwona mchumba wake
mtarajiwa.
Uchunguzi huu hufanyika bila wanawake
wenzie kujua kwa hiyo mwanaume anayeonekana kuchangamkiwa sana na
wanawake wenzake kwa lengo la kumvuta ili awe mpenzi wake ndiye ambaye
atapata uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na mwanamke huyo.
No comments:
Post a Comment